Na hakika tumewatukuza wanaadamu, na tumewapa vya kupanda nchi kavu na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na tumewafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa tulio waumba. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Kwa hakika tumewatukuza watu wa kizazi cha Ādam kwa akili na kuwapelekea Mitume, na tukawadhalilishia vilivyoko ulimwenguni vyote: tukawadhalilishia wanyama barani wa kuwapanda na vyombo baharini vya kuwabeba, tukawaruzuku vilaji na vinywaji vizuri na tukawapa daraja kubwa juu ya viumbe wengi.